Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kampeni za Uchaguzi Uganda zasimamishwa

72ea24a6b61e474ceb00bb5f05c9225b Kampeni za Uchaguzi Uganda zasimamishwa

Sun, 3 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

Tume ya Uchaguzi nchini Uganda imesimamisha kampeni katika maeneo ya mijini yenye idadi kubwa ya watu kutokana na kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya corona (COVID-19.

Wilaya zilizozuiwa kufanya Kampeni ni Mbarara, Kabarole, Luwero, Kasese, Masaka, Wakiso, Kabarole, Jinja, Kalungu, Kazo and Tororo.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo, Simon Mugenyi kampeni zimepigwa marufuku katika maeneo hayo hadi itakapotangazwa tena mara baada ya tume kukutana na wataalamu wa afya siku za hivi karibuni ili kupata ufumbuzi wa tatizo hilo.

Chanzo: habarileo.co.tz