Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kampeni ya chanjo ya MPOX kuanza mwezi ujao DRC

Vaccine Mpox.jpeg Kampeni ya chanjo ya MPOX kuanza mwezi ujao DRC

Mon, 9 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kampeni ya chanjo dhidi ya homa ya Mpox katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo itaanza inatarajiwa kuanza Oktoba 2.

Hayo yameelezwa na mamlaka husika nchini humo huku wafanyakazi wakilenga majimbo matatu yaliyoathirika zaidi.

Watu wazima katika majimbo ya Equateur, Kivu Kusini na Sankuru watapewa chanjo ya kwanza, Cris Kacita Osako, mratibu wa Kamati ya Majibu ya Monkeypox ya Congo, ameziambia duru za Habari.

Mapema wiki hii, kundi la kwanza la chanjo ya mpox liliwasili katika mji mkuu wa Congo, kitovu cha mlipuko huo.

Dozi 100,000 za chanjo ya JYNNEOS, iliyotengenezwa na kampuni ya Denmark ya Bavarian Nordic, ilitolewa na Umoja wa Ulaya kupitia HERA, wakala wa kambi hiyo kwa dharura za afya. Dalili kuu ya homa ya MPOX ni kutokwa na vipele vikubwa

Nyingine 100,000 zilitolewa Jumamosi ya juzi. Dozi 200,000 ni sehemu tu ya dozi milioni 3 ambazo mamlaka zimesema zinahitajika kumaliza milipuko ya mpox nchini Kongo.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yenye watu zaidi ya milioni 100 iko kwenye kitovu cha mlipuko wa mpox ugonjwa ambao Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitangaza kuwa ni dharura ya afya ya umma duniani mwezi uliopita.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani - WHO, karibu visa 15,000 vya mpox vimegundulika nchini Kongo katika mwaka wa 2024, huku kukiwa na vifo 500.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa, licha ya kuwa maambukizi ya ugonjwa huo yamekuwa yakiongezeka kwa kasi, lakini vifo vinavyotokana na maradhi hayo ni vichache.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live