Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kamera zapigwa 'stop' kwenye mahafali Uganda

Mahafali Mahafali Kamera zapigwa stop kwenye mahafali Uganda

Mon, 13 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Moja ya vyuo vikuu vya hadhi barani Afrika kimepiga marufuku wanaohudhuria sherehe za kuhitimu kubeba simu, kamera za video, kwa mujibu wa taarifa.

Chuo kikuu cha Makerere nchini Uganda kuanzia Jumatatu kitafanya sherehe ya kuhitimu ya siku tano kwenye Uwanja wake wa Freedom Square

Jumla ya wanafunzi 13,221 wamepangwa kuhitimu, huku kila mmoja akiruhusiwa kualika wageni wawili pekee.

Hakuna sababu iliyotolewa ya kupigwa marufuku kwa kamera katika uwanja wa mahafali, lakini vitu vingine vilivyopigwa marufuku kwenye sherehe hiyo ni pamoja na pombe, sigara, vyakula vya makopo na vinywaji vya chupa.

"Orodha ya kina ya bidhaa zilizopigwa marufuku imeingizwa kwenye kifurushi cha mialiko ya kuhitimu ambayo huwasilishwa kwa wahitimu na wageni waalikwa," mkuu wa kamati ya sherehe, Prof Patrick Mangeni, alisema.

Mke wa Rais Janet Museveni, ambaye pia ni waziri wa elimu ya msingi, anatarajiwa kuhudhuria sherehe hiyo siku ya Jumatatu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live