Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kamera za mnasa Raila akiponda raha Mombasa

Ad821cdb2c1f0d75 Kamera za mnasa Raila akiponda raha Mombasa

Fri, 17 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Raila Odinga kwa sasa yuko likizoni Kaunti ya Mombasa kwa siku tatu, ili kujipumzisha baada ya miezi kadhaa ya kufanya kampeni za siasa Mnamo Alhamisi, Disemba 16, kinara huyo wa ODM alimtembelea Francis Atwoli kwenye nyumba yake ya kifahari iliyoko Kilifi, ambako walibaziri wakinywa kahawa huku wakitazama bahari ya kuvutiaPicha hiyo iliibua mjadala kwenye mitandao ya kijamii, huku wengi wakikiri kwamba ni dhahiri shahiri wawili hao wanaishi kwa tunu na tamasha Picha ya kinara wa ODM Raila Odinga akijivinjari na Katibu Mkuu wa Vyama vya Wafanyakazi Nchini (COTU) Francis Atwoli wakiwa katika Kaunti ya Kilifi, imeibua mjadala miongoni mwa Wakenya.

Waziri mkuu huyo wa zamani yuko likizoni katika maeneo ya Pwani baada ya kushauriwa achukue mapumziko mafupi, kufuatia misururu ya mikutano za siasa akipiga kampeni za kiti cha urais 2022.

Kwenye picha hiyo ilisambazwa na Atwoli, viongozi hao wawili wanaonekana wakiburudika kwa kikombe cha kahawa kwenye nyumba ya kifahari ya mkuu huyo wa COTU iliyoko Bofa Ocean View, Kilifi.

Read also

Sabina Chege Aapa Kumpigia Debe Raila 2022 Hata Kama Atapoteza Kiti Chake

Wawili hao wanatazama bahari iliyoko mbele yao huku wakizidi kujinafas kwa raha zao.

"Tunakunywa kikombe cha kahawa tukiwa na Baba @RailaOdinga nyumbani kwangu Bofa Ocean View iliyoko Kilifi. Ni wakati mzuri wa kutafakari," Atwoli alisema.

Picha hiyo ilizua hisia mseto kwenye mitandao ya kijamii huku wengi wakikubali kuwa, wawili hao wanaishi maisha ya kifahari.



Awali TUKO.co.ke iliripoti kuwa, Raila alishauriwa achukue mapumziko baada ya kuhudhuria misururu ya mikutano ya siasa kote nchini.

"Niko Mombasa kupumzika kwa siku tatu. Sijaanda mkutano wowote leo. Nilishauriwa nipumzike baada ya hafla ya Kasarani. Baada ya siku tatu nitafanya mazungumzo na watu mbali mbali pamoja na vikundi," Raila alisema.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live