Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kamati ya kijeshi Libya yakutana baada ya miezi 7

Bendera Lkukutanaaa Kamati ya kijeshi Libya yakutana baada ya miezi 7

Mon, 16 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamati ya pamoja ya kijeshi ya 5+5 ya Libya jana Jumapili ilikutana kwa mara ya kwanza baada ya kupita miezi saba na kujadili masuala kadhaa, ikiwa ni pamoja na kusitisha mapigano katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.

Kamati hiyo imefanya mkutano huo katika mji wa pwani wa Sirte na kumshirikisha pia mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya.

Kamati hiyo inajumuisha wajumbe watano kutoka serikali ya umoja wa kitaifa yenye makao yake makuu mjini Tripoli na watano kutoka vikosi vya Khalifa Haftar.

Meja Jenerali Khaled Mahjub, kiongozi wa Kikosi cha Mashariki mwa Libya kinachoongozwa na Haftar, amethibitisha habari hiyo katika taarifa yake na kuongeza kwamba, kwamba Abdoulaye Bathily, Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya naye ameshiriki katika mkutano wa kamati hiyo uliofanyika katika mji wa bandari wa Sirte.

Wajumbee katika mkutano huo wamejadiliana vifungu vya makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyotiwa saini huko Geneva Uswiwi mwaka 2020, pamoja na kazi ya waangalizi wa kimataifa na wa ndani juu ya makubaliano hayo.

Pia waligusia masuala ya kuunganishwa taasisi za kijeshi nchini humo na kufukuzwa askari wa kigeni na mamluki wa madola ajinabi. Kamati hiyo ilikutana mara ya mwisho mwezi Juni 2022 katika mji mkuu wa Misri, Cairo.

Miongoni mwa matunda muhimu ya makubaliano ya mwezi Oktoba 2020 ni makubaliano ya kudumu ya kusitisha mapigano yaliyotiwa saini kati ya serikali ya Libya na wajumbe walio na uhusiano na Jenerali Haftar.

Libya imekumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu kung'olewa madarakani mtawala wa muda mrefu Muammar Gaddafi mwaka 2011.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live