Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kamanda wa waasi wa Lord's Resistance Army ya Uganda ashtakiwa

Kamanda Wa Waasi Wa Lord's Resistance Army Ya Uganda Ashtakiwa Kamanda wa waasi wa Lord's Resistance Army ya Uganda ashtakiwa

Fri, 19 Jan 2024 Chanzo: Bbc

Kesi iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu ya mtoto mwanajeshi aliyegeuka kamanda wa kundi la Lord's Resistance Army (LRA) imeanza kusikilizwa nchini Uganda.

Thomas Kwoyelo anakabiliwa na mashtaka zaidi ya 90 - ikiwa ni pamoja na mauaji, ubakaji na kuajiri watoto askari.

Anakuwa kamanda wa kwanza wa LRA kuhukumiwa na mahakama ya Uganda, na kuashiria wakati mgumu kwa mfumo wa mahakama nchini humo.

Wakati wa kufikishwa mahakamani mwaka wa 2011, Bw Kwoyelo alikanusha mashtaka dhidi yake.

Ametumia miaka 14 iliyopita kizuizini kabla ya kesi, ambayo wachambuzi kwa sehemu wanahusisha ukubwa na utata wa uhalifu unaodaiwa.

Joseph Kony aliunda LRA nchini Uganda zaidi ya miongo miwili iliyopita, na alidai kuwa anapigania kuunda serikali inayozingatia Amri 10 za Biblia.

Kundi hilo lilikuwa maarufu kwa kuwakata watu miguu na mikono na kuwateka nyara watoto ili kuwatumia kama wanajeshi na watumwa wa ngono. Mamia ya maelfu ya watu walilazimishwa kutoka makwao kutokana na mzozo huo.

Iilihudumu zaidi kaskazini mwa Uganda mwanzoni, kisha likahamia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambako Bw Kwoyelo alikamatwa mwaka wa 2009, na baadaye Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Kesi ya Ijumaa inasikilizwa katika Kitengo cha Uhalifu wa Kimataifa cha Mahakama Kuu ya Gulu, inayoonekana kama jibu la Uganda kwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu huko The Hague.

Bw Kwoyelo aliwahi kufika kortini kama sehemu ya vikao vya kusikilizwa kwa kesi hiyo, lakini kesi hiyo imeahirishwa mara kadhaa.

Mashahidi wengi wanatarajiwa kutoa maelezo yao ya kile kilichotokea mahakamani.

Human Rights Watch hapo awali ilikosoa ucheleweshaji wa kesi hii, na inasema kwa ujumla kumekuwa na uwajibikaji mdogo kwa uhalifu uliofanywa wakati wa mzozo wa miaka 25 ikiwa ni pamoja na unyanyasaji wa vikosi vya serikali ya Uganda.

Mnamo 2021, kamanda mkuu wa LRA Dominic Ongwen alifungwa jela miaka 25 na ICC, ambayo iliamua kutompa kifungo cha juu cha maisha kwa sababu alitekwa nyara akiwa mtoto na kufundishwa na waasi waliowaua wazazi wake.

Bw Kwoyelo anasema yeye pia alitekwa nyara na wapiganaji wa LRA katika miaka yake ya ujana alipokuwa akienda shule.

Maelfu ya wanachama wa zamani wa LRA wamepewa msamaha chini ya sheria tata ya Uganda, baada ya kuondoka na kulikana kundi hilo la waasi.

Lakini chaguo hili halikutolewa kwa Bw Kwoyelo, na hivyo kusababisha shutuma kuwa kukanusha kulichochewa kisiasa.

Wakati kesi yake ikiendelea, kuna wasiwasi kwamba ufadhili huo unaweza kuisha, na kusababisha ucheleweshaji zaidi kwa haki

Chanzo: Bbc