Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kamanda wa kijeshi Sudan amuunga mkono kiongozi wa mapinduzi

SUDAN22 Kamanda wa kijeshi wa Sudan amuunga mkono kiongozi wa mapinduzi

Mon, 8 Nov 2021 Chanzo: BBC

Kamanda wa kijeshi wa Sudan, Mohamed Hamdan Dagalo, anayejulikana kwa jina la Hemeti, ameunga mkono hatua ya Jenerali Abdel Fattah al-Burhan kuchukua madaraka.

Hemeti, ambaye alikuwa naibu kiongozi katika Baraza la Utawala lililovunjwa sasa, alisema Jenerali Burhan "alikuja kusahihisha mwenendo wa mapinduzi, na kulinda usalama na utulivu wa nchi".

Maandamano ya kupinga mapinduzi hayo yamekuwa yakiendelea, ingawa ushiriki wa Jumapili uliripotiwa kuwa mdogo kwa sababu ya kukatika kwa mtandao.

Maafisa wa usalama waliwarushia vitoa machozi waandamanaji na baadhi ya walimu waliokuwa wakiandamana walizuiliwa.

Waandamanaji wanataka kukomeshwa kwa utawala wa kijeshi baada ya Jenerali Burhan kuvunja utawala kiraia wa serikali.

Chanzo: BBC