Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kamanda mkuu wa ADF, wapiganaji 3 wauawa DR Congo

Kamanda Mkuu Wa ADF, Wapiganaji 3 Wauawa DR Congo Kamanda mkuu wa ADF, wapiganaji 3 wauawa DR Congo

Sun, 27 Aug 2023 Chanzo: Bbc

Wanajeshi wa Uganda Pamoja na wenzao wa DR congo wamefanikiwa kumuua kamanda mmoja wa kundi la ADF pamoja na wapiganaji wengine watatu kwa mujibu wa mamlaka siku ya Ijumaa kwa mujibu wa mtandao wa The Monitor nchini humo.

‘’Jeshi la Muungano la wanajeshi wa UPDF likishirikiana na wanajeshi wa DR congochini ya operesheni ya shujaa hii leo ilimuua kamanda mmoja wa wapiganaji wa ADFkwa jina fazul ambaye alikuwa alitekeleza opresheni zake katika Bonde la Mwalika’’, alisema msemaji wa UPDFMeja Bilala Katamba.

Kulingana na jeshi hilo, kamanda aliyeuawa alikuwa raia wa Tanzania . Aliuawa pamoja na mpiganaji mmoja wa ADF katika mkoa wa Kivu kaskazini nchini Dr Congo.

Tarehe 23 mwezi wa nane 2023, Vikosi vinavyoshirikiana chini ya UPDF3 katika eneo la Kanana, Makisabo, Kivu kaskazini pia vilifanikiwa kuwaua wapiganaji wawili wa ADFna kupata silaha kadhaa mbali na Radio moja ya kijeshi, alisema Meja Katamba katika taarifa kwa vyombo vya habari siku ya Ijumaa.

Mwaka 2021 , wanajeshi wa Uganda walipelekewa nchini DR Congo katika operesheni iliozinduliwa dhidi ya wapiganaji wa ADF.

Chanzo: Bbc