Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kalonzo asema yuko huru kufanya kazi na Ruto au Raila

9d20009fed098c23 Kalonzo asema yuko huru kufanya kazi na Ruto au Raila

Sat, 6 Nov 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka amesema yuko tayari kufanya kazi na Raila Odinga au naibu rais William Ruto katika kuunda serikali ijayo.

Kalonzo alisema hajawahi kuwa na kikao na Raila kujadili siasa za 2022 na uwezekano wa kufanya kazi pamojaAlisema yuko tayari kukutana na Raila au Ruto iwapo wanataka kuwa na makubaliano naye kuhusu uchaguzi ujao.

Kalonzo amekuwa kwenye muungano wa OKA lakini sasa anasema yuko huru kujenga muungano na wengine.

Kalonzo alikuwa mgombea mwenza wa Raila kwenye muungano wa NASA katika kinyang'anyiro cha 2017.

Alisema anaweza kuungana tena na Baba katika uchaguzi wa 2022 lakini akasema atafanya hivyo kukiwa na sababu murwa.

"Kumuunga mkono kwa mara ya tatu italazimu kuwe na sabbau nzuri. Ndio maana nilisema nikifanya hivyo nitakuwa mjinga. Iwapo nitafanya hivyo basi lazima niwe na sababu mzuri, iwapo tutafika hapo basi kutakuwa na mazungumzo," alisema Kalonzo.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke