Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kalonzo aahidi elimu ya bure kama OKA wataunda serikali 2022

0fgjhs3fkh6rn9j2jg Kalonzo aahidi elimu ya bure kama OKA wataunda serikali 2022

Sun, 7 Nov 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka alikuwa akizungumza katika shamba lake lililoko eneo la Yatta alipowahutubia wanawake wa vikundi 12 mbalimbali vya wanawake wa kutoka Mt KenyaKalonzo aliwahimiza kina mama hao kuunga mkono muungano wa One Kenya Alliance (OKA)Kalonzo alisema kwamba nchi hii inahitaji kuwekeza katika elimu bora kuanzia shule ya msingi hadi vyuoni Kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka alisema kwamba kutakuwapo na elimu ya bure ya sekondari humu nchini iwapo muungano wa One Kenya Alliance (OKA) utaunda serikali ijayo.

Akizungumza mnamo Ijumaa Novemba 5 akiwa shambani kwake eneo la Yatta wakati alipowahutubia msafara wa vikundi vya kina mama katika kaunti 12 za eneo la Mt. Kenya, Kalonzo alisema kwamba nchi hii inahitaji kuwekeza katika elimu bora kuanzia shule za msingi hadi vyuo vikuu.

Aliwapa kina mama hao maneneo matamu huku akisema kwamba alihusika pakubwa katika kufanikisha uongozi wa rasi mstaafu Mwai Kibaki kuanzia mwaka wa 2002 hadi 2013.

“Mimi nilikuwa mshauri mkubwa wa Kibaki na mambo ya elimu ya msingi bila malipo si ilifanyika..sasa nitahakikisha OKA ikiingia Wiper ikiwa mbele basi kutakuwa na elimu ya sekondari bila malipo...na kisha tutafanya "value addition" kwa bidhaa kama kabichi ya Nyandarua,” Kalonzo alisema.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke