Mahakama nchini Algeria imemuhukumu kaka wa Rais wa zamani wa nchi hiyo Abdelaziz Bouteflika kifungo cha miaka 12 jela kwa rushwa.
Said Bouteflika ambaye alikuwa akifanya kazi kama mshauri wa kaka yake pia ametakiwa kulipa faini ya dola za Kimarekani takribani 60,000.
Katika kesi hiyo hiyo, wafanyabiashara wengine wakubwa nchini humo nao wamehukumiwa vifungo vya muda mrefu pamoja.
Rais Abdelaziz Bouteflika ambaye alikuwa akituhumiwa kuzidisha rushwa wakati wa utawala wake wa miaka 20 alilazimika kujiuzulu Urais mwaka 2019 baada ya wimbi la maaandamano ya kuunga mkono demokrasia.
Alifariki miaka miwili baadaye.