Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kahawa ya Tanzania kuonjwa China siku 5

926e88b34d5d897273a5151fce7f9c07.jpeg Kahawa ya Tanzania kuonjwa China siku 5

Mon, 17 May 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MAMLAKA ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) imesema kahawa ya Tanzania itatangazwa kwenye soko la China kwa siku tano.

Taarifa ya Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa TanTrade, Daniel Biah, alisema Ubalozi wa Tanzania nchini China unaratibu hafla ya kuonja kahawa ya Tanzania inayotarajiwa kufanyika Juni 14 hadi 18 mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo kwa umma, ubalozi utashirikiana na Idara ya Biashara ya Jimbo la Hunan na kampuni zinazonunua kahawa nchini China.

Biah alisema kampuni zinazonunua kahawa kutoka sehemu mbalimbali duniani zinatarajiwa kuhudhuria hafla hiyo jijini Changsha.

Tantrade ilieleza kuwa hafla hiyo ni sehemu ya matukio ya awali kabla ya Maonesho ya Biashara na Uchumi ya China na Afrika yanayotarajiwa kufanyika Septemba mwaka huu.

“Wazalishaji na wauzaji wa kahawa nchini wanahimizwa kushiriki halfa hiyo ili kutangaza kahawa ya Tanzania kwa kutuma sampuli za kahawa kwa ajili ya zoezi la uonjaji,” alieleza taarifa hiyo.

Biah alizitaja sampuli zinazohitajika kuwa ni ‘washing bean,’ ‘nitro dry bean,’ ‘anaerobic process bean,’ ‘honey white yellow black bean,’ ‘red wine treatment bean.’

Chanzo: www.habarileo.co.tz