Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kagame ashinda urais wa Rwanda kwa kishindo

Kagame Election Kagame ashinda urais wa Rwanda kwa kishindo

Tue, 16 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mgombea Urais wa Chama cha RFP, Paul Kagame ameshinda tena kiti hicho baada ya kupata kura 7,099,810 sawa na asilimia 99.15 ya kura zote zilizopigwa ambazoni 9,071,157.

Kagame amewashinda Frank Habineza wa Chama cha Democratic Green aliyepata jumla ya kura 38,301 sawa na asilimia 0.53 na Phillipe Mpayimana aliyepata kura 22,753 sawa na asilimia 0.32.

Wananchi wa Rwanda leo Jumatatu, Julai 15, 2024, wamepiga kura katika Uchaguzi Mkuu wao ikiwa ni mara ya nne tangu yatokee mauaji ya kimbari mwaka 1994. Kura za ubunge zinaendelea kuhesabiwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live