Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kagame amshutumu Tshisekedi kutafuta sababu ya Rwanda kuahirisha uchaguzi Congo

Kagame Amshutumu Tshisekedi Kutafuta Sababu Ya Rwanda Kuahirisha Uchaguzi Congo Kagame amshutumu Tshisekedi kutafuta sababu ya Rwanda kuahirisha uchaguzi Congo

Thu, 1 Dec 2022 Chanzo: Bbc

Rais wa Rwanda Paul Kagame amemshutumu mwenzake wa DR Congo kwa "kujaribu kutafuta njia ya kuahirisha uchaguzi ujao"kwa kuihusisha Rwanda katika mgogoro wa mashariki mwa Congo.

Kinshasa haijajibu mara moja matamshi ya Bw Kagame ambaye bila kuwasilisha ukweli alisema rais wa Congo hakushinda "uchaguzi wa kwanza".

Katika hotuba ndefu nadra siku ya Alhamisi katika Bunge la Rwanda, Rais Kagame alisema ni "aibu" kwamba vyama vingi na nchi "zinadai kutaka kutatua tatizo hilo", lakini "hazijapata suluhu kwa miongo kadhaa sasa".

Bw Kagame alizionya nchi zenye nguvu, akitaja Marekani, Uingereza, Ufaransa, na Umoja wa Mataifa kwa kushutumu au kuamini kwamba Rwanda ndiyo inayohusika na machafuko mashariki mwa Congo, huku akishutumu vikosi vya Umoja wa Mataifa kwa kushindwa kulitokomeza kundi la waasi la Rwanda la FDLR na wengine.

Pia alikanusha madai kwamba Rwanda ilikuwa ikiiba madini kutoka Congo, "kitu kimoja ambacho sisi sio, sisi sio wezi" alisema.

Alisema madini mengi ya Congo "yalisafirishwa kwa magendo au kupitia njia sahihi" kupitia Rwanda hadi Dubai, Brussels, au Tel Aviv, na Urusi.

"Wanatutuhumu kwa kuiba madini ya Congo vipi kuhusu sehemu yalikowasilishwa? " alihoji.

Bw Kagame alisema Rwanda haiko katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kwamba waasi wa M23 sio Wanyarwanda bali ni wa Congo, akilaumu uasi wao kwa serikali ya Kinshasa kwa kutoheshimu makubaliano ya awali na kundi hilo.

Kwa kuihusisha Rwanda, Kagame alimshutumu Bw Tshisekedi, kwamba alikuwa akitengeneza "visingizio vya dharura ili uchaguzi (mwaka ujao) usifanyike".

"Sawa, si kwamba alishinda uchaguzi wa kwanza kama tunavyojua, kama anajaribu kutafuta njia nyingine ya kuahirisha uchaguzi ujao basi ni afadhali atumie visingizio vingine sio sisi", aliongeza bila kuwasilisha ukweli wa madai yake.

Bw Kagame alisema Rwanda inaweza kusaidia katika kushughulikia tatizo la M23 na makundi mengine ya waasi mashariki mwa Congo.

"Kwa sababu tuna nia ya kuwa na ujirani mwema," alisema.

Chanzo: Bbc