Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kagame akubali kukutana na Tshisekedi mzozo wa mashariki mwa DRC

Kagame Akubali Kukutana Na Tshisekedi Kuhusu Mzozo Wa Mashariki Mwa DRC Kagame akubali kukutana na Tshisekedi kuhusu mzozo wa mashariki mwa DRC

Tue, 12 Mar 2024 Chanzo: Bbc

Rais wa Rwanda Paul Kagame amekubali kukutana na mwenzake wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi kujadili mzozo unaoendelea mashariki mwa Congo, serikali ya Angola imesema.

Makubaliano hayo yalifuatia mkutano wa Jumatatu katika mji mkuu wa Angola Luanda kati ya Bw Kagame na Rais wa Angola João Lourenço, mpatanishi wa Umoja wa Afrika (AU) katika mgogoro wa DR Congo.

"Iliamuliwa kuwa Rais Kagame atakubali kukutana na Rais Tshisekedi katika tarehe itakayowekwa na mpatanishi," Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola Tete Antonio aliambia wanahabari baada ya mkutano huo.

Bw Antonio alisema kuwa Rwanda na DR Congo zimekubali kufanya mkutano huo, huku wajumbe wa mawaziri kutoka pande zote mbili wakishughulikia mpango huo.

Ofisi ya rais wa Rwanda ilisema kwenye mtandao wa X kwamba viongozi hao wawili "walikubaliana juu ya hatua muhimu za kushughulikia sababu kuu za mzozo".

Safari ya Rais Kagame nchini Angola inafuatia ziara kama hiyo ya Bw Tshisekedi mjini Luanda mwezi uliopita, ambapo ilitangazwa kuwa kiongozi huyo wa DR Congo amekubali kukutana na mwenzake wa Rwanda.

Lakini Bw Tshisekedi alidai kuondolewa kwa wanajeshi wa Rwanda katika eneo la Congo kabla ya kukutana na Rais Kagame, ofisi ya rais wa DR Congo ilisema.

Mapigano kati ya waasi wa M23 na wanajeshi wa Congo yamepamba moto mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na kusababisha zaidi ya watu 100,000 kuyahama makazi yao katika wiki za hivi karibuni, kulingana na UN.

DR Congo imeishutumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa M23, tuhuma ambayo Kigali inakanusha.

Chanzo: Bbc