Thu, 15 Dec 2022
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Rais wa Rwanda, Paul Kagame amesema Rwanda haikuunda tatizo la Congo na haiwezi kuwajibika kwa matatizo yanayosababishwa na Wakongo wenye asili ya Rwanda wanaodai kunyimwa Haki zao huko.
Kauli ya Kagame inakuja kukiwa na ongezeko la vifo na Umwagaji Damu katika Maeneo yanayokaliwa na Waasi wanaoaminika kuwa na Silaha na kuungwa Mkono na #Rwanda, Ingawa Kagame amekanusha hilo.
Umoja wa Mataifa ulifanya Uchunguzi Novemba 2022 na kubaini Wanaume, Wanawake na Watoto 131 waliuawa kwa kupigwa Risasi na kukatwakatwa hadi kufa ikitajwa kuwa ni kisasi dhidi ya Raia na Waasi wa M23.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live