Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kagame ailaumu jamii ya kimataifa mauaji ya kimbari ya Rwanda

Kagame Kimbari.png Kagame ailaumu jamii ya kimataifa mauaji ya kimbari ya Rwanda

Mon, 8 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Paul Kagame wa Rwanda ameilaumu jamii ya kimataifa kwa kutochukua hatua za kuzuia mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini humo. Rais Kagame alibainisha haya jana wakati Wanyarwanda walipoadhimisha miaka 30 tangu kujiri mauaji hayo ya kutisha ambapo Wahutu wenye misimamo mikali waliwauwa Watutsi wasiopungua laki nane.

Katika maadhimisho hayo ya kumbukumbu ya mauaji ya kimbari ya Rwanda, Rais Paul Kagame ameeleza kuwa Rwanda imepata ahueni kubwa na ukuaji wa uchumi miaka kadhaa baada ya mauaji ya kimbari lakini bado makovu yamesalia.

Katika shughuli hiyo ya kumbukumbu ya mauaji ya kimbari iliyofanyika mjini Kigali, Rais Kagame aliongoza shughuli ya maadhimisho ya kutimia miaka 30 tangu kujiri mauaji ya mwaka 1994 ambayo ilihudhuriwa na wageni na viongozi mbalimbali wa sasa na wastaafu kutoka pembe mbalimbali duniani wakiwemo rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton, Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa na wengine wengi. Bill Clinton na Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa katika marasimu ya miaka 30 ya mauaji ya kimbari Rwanda

Kwa muda mrefu sasa serikali ya Rwanda imekuwa ikiilaumu jamii ya kimataifa kuwa ilipuuza tahadhari kuhusu mauaji hayo; ambapo hadi sasa baadhi ya viongozi wa nchi za Magharibi wameeleza kujutia na kusitikishwa na mauaji ya kimbari ya Rwanda.

Itakumbukwa kuwa, Bill Clinton baada ya kumaliza muhula wake wa uongozi nchini Marekani aliyataja mauaji ya kimbari ya Rwanda kuwa ni kushindwa kwa uongozi wake. Aidha Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema katika video iliyorushwa jana Jumapili kabla ya maadhimisho ya miaka 30 ya mauaji ya kimbari ya Rwanda kwamba Ufaransa na waitifaki wake wangeweza kuzuia kutokea mauaji hayo hata hivyo hawakuwa na nia ya kufanya hivyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live