Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kagame, Tshisekedi wawasili kenya

Wawasili Rwanda Congo Kenya.png Kagame, Tshisekedi wawasili kenya

Mon, 20 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambaye pia ni Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amewapokea Marais sita kati ya saba wa Mataifa saba ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao wamekutana leo Jumatatu Jijini Nairobi, Kenya kujadili hali ya usalama katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Mkutano huo unakuja wakati kumezuka mapigano makali yanayofufua uhasama wa miongo kadhaa kati ya Congo na Rwanda, huku DRC ikiilaumu Rwanda kutokana na kuibuka upya kwa kundi la Waasi la M23.

Marais waliohudhuria mkutano huo ni Kenyatta wa Kenya, Yoweri Museveni (Uganda), Paul Kagame (Rwanda), Evariste Ndayishimiye (Burundi), Salva Kiir Mayardit (South Sudan) na Felix Tshisekedi (DR Congo).

Rais wa Tanzania Samia Suluhu amewakilishwa kwenye mkutano huo na Balozi wa Tanzania nchini Kenya, John Simbachawene.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live