Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kagame: Rwanda haitapokea wakimbizi wa DR Congo

Kagame: Rwanda Haitapokea Wakimbizi Wa DR Congo Kagame: Rwanda haitapokea wakimbizi wa DR Congo

Tue, 10 Jan 2023 Chanzo: bbc

Rais wa Rwanda, Paul Kagame anasema nchi yake haitatoa tena hifadhi kwa watu wanaokimbia migogoro katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Miongo kadhaa ya ukosefu wa utulivu mashariki mwa DRC imelazimisha wakimbizi wengi kuvuka mpaka na kuingia Rwanda.

"Hili si tatizo la Rwanda," alisema Bw Kagame na kuongeza:

"Ninakataa kwamba Rwanda inapaswa kubeba mzigo huu." Dunia nzima imeshindwa kuelewa tatizo na kuingia mashariki mwa DR Congo alisema Kagame.

Tishio halisi kwa usalama - kwa maoni yake - ni kile anachoelezea kama mabaki ya vikosi vya Wahutu wenye itikadi kali ambao walijaribu kuliangamiza kabila lake la Kitutsi katika mauaji ya kimbari ya 1994.

Rwanda inashutumiwa kwa kuunga mkono kundi la waasi la M23 - jambo ambalo nchi hiyo imekuwa ikikanusha.

Kundi hilo la waasi limeteka maeneo mengi katika miezi ya hivi karibuni, na kutuma makumi ya maelfu ya wakimbizi kuvuka mpaka na kuingia Rwanda.

Chanzo: bbc