Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kagame: Rwanda haijahusika kivyovyote na mapigano mashariki ya DRC

Kagame Drc Rwanda Kagame: Rwanda haijahusika kivyovyote na mapigano mashariki ya DRC

Wed, 24 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Rwanda, Paul Kagame amesema nchi hiyo haijahusika kivyovyote na mapigano na ghasia zinazoendelea kushuhudiwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Rais Kagame alisema hayo jana Jumanne na kuongeza kuwa, "Rwanda haikuanzisha vita vinavyoshuhudiwa mashariki ya Congo, huu ndio ukweli na uhalisia wa mambo."

Kagame amebainisha kuwa, kwa muda mrefu sasa, kumekuwa na jitihada za kutaka kuionesha dunia kwamba Rwanda ndiyo iliyoanzisha na kuchochea vita hivyo.

"Nendeni mfanye uchunguzi na mtabaini kuwa hakuna mkono wa Rwanda katika vita hivyo vinavyoshuhudiwa mashariki ya DRC," ameongeza Rais Paul Kagame.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imekuwa ikimtuhumu jirani yake huyo Rwanda kuwa inaliunga mkono kundi la waasi wa M23, madai ambayo yamekanushwa na Kigali, lakini yanaungwa mkono na Marekani, Ufaransa, Ubelgiji na wataalamu wa Umoja wa Mataifa.

Mvutano kati ya majirani hao uliongezeka tangu kuzuka upya kwa harakati za wanamgambo wa M23 mwishoni mwa 2021 mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Wanamgambo wa M23 mashariki ya DRC

Mwezi uliopita wa Disemba, Rais Felix Tshisekedi wa DRC akihutubia umati wa wafuasi wake katika mkutano wa kampeni za uchaguzi wa rais mashariki mwa nchi, alimshabihisha mwenzake huyo wa Rwanda, Paul Kagame na mtawala wa zamani wa Ujerumani ya Manazi, Adolf Hitler.

Aidha alisema wakati wa kampeni hizo kwamba, akichaguliwa tena kuwa rais wa DRC, ataomba ridhaa ya Bunge na Kongresi atangaze vita dhidi ya Rwanda. Tshisekedi aliapishwa Jumamosi iliyopita kwa muhula wa pili wa miaka mitano, baada ya Mahakama ya Katiba kuthibitisha ushindi wake katika uchaguzi mkuu wa mwezi Desemba mwaka jana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live