Rais wa Rwanda, Paul Kagame amesema hakuna Chombo chochote kutoka nje ya Nchi hiyo ambacho kinaweza kuiamuru Rwanda njia ipi ipite na kuuamuru Uongozi nini cha kufanya ambapo amesema jukumu hilo ni la Watu wa Rwanda wenyewe.
Akiongea wakati wa maombi y Kitaifa Nchini humo, Kagame amesema “Watu wote tupo sawa mbele za Mungu hakuna Mtu ambaye yupo juu kuliko mwingine, ukweli huu uwe chanzo cha kuwapa hamasa na msukumo utakaowapa mwongozo wa matendo yenu kwenye masuala mbalimbali”
“Kwa kuizingatia historia ya Rwanda, changamoto tunazozipitia sasa na malengo yetu ya baadaye, ni dhahiri kwamba hakuna Chombo chochote kutoka nje bila kujali asili yake ambacho kinaweza kutuamrisha njia ipi Nchi yetu ipite, kutuamrisha Uongozi wetu uweje na wapi tuelekee, jukumu hilo ni letu sisi Watu wa Rwanda wenyewe”
“Haijalishi unatokea wapi lakini kama una maoni mazuri ambayo yanatofautiana na yangu nitakusikiliza na tutafanya mazungumzo lakini siwezi kukubali amri ya Mtu yoyote kutoka kwa wale wanaodhani ni bora kuliko sisi sote na wanaodhani wana haki kwenye huu utawala, siwezi kukubali “