Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kabuga kuamua ni wapi ataishi atakapoachiliwa - Mwendesha mashitaka mkuu

Kabuga Kuamua Ni Wapi Ataishi Atakapoachiliwa   Mwendesha Mashitaka Mkuu Kabuga kuamua ni wapi ataishi atakapoachiliwa - Mwendesha mashitaka mkuu

Thu, 10 Aug 2023 Chanzo: Bbc

Félicien Kabuga, ambaye anatuhumiwa kwa makosa ya mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994, alipokuwa akifuatilia kesi hiyo, alikuwa katika gereza la mahakama ya The Hague Machi 30 (3) mwaka huu.

Félicien Kabuga, ambaye anashukiwa kwa uhalifu wa mauaji ya halaiki nchini Rwanda mwaka 1994, ataamua kuhusu nchi anayotaka kuishi maisha yake yote, atakapoachiliwa.

Lakini Serge Brammertz, mwendesha mashtaka mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) chemba (chumba) ambacho kilipewa jukumu la kuendesha kesi za jinai zilizoachwa na mahakama za Umoja wa Mataifa, alisema kwamba itategemea kama nchi yoyote inataka kumpokea.

Brammertz aliiambia BBC Focus on Africa: "Bila shaka ni juu ya utetezi kuangalia nchi na watu wa kuzungumza nao [kuihusu].

"Lakini ingewezekana tu ikiwa kungekuwa na ruhusa ya nchi ya tatu".

Kabuga alizaliwa katika manispaa ya Mukarange katika wilaya ya zamani ya Byumba, sasa katika wilaya ya Gicumbi katika jimbo la kaskazini mwa Rwanda.

Alikamatwa nchini Ufaransa, katika eneo la Asnières-sur-Seine, karibu na mji mkuu wa Paris, Mei 16 (5), 2020, ambapo alikuwa akiishi kwa kutumia kitambulisho cha kijamii katika makazi ya hosteli ya ndani, kama ilivyotangazwa na Wizara ya Sheria ya Ufaransa.

Imepita miaka 25 tangu asakwe na mahakama ya kimataifa.

Hawezi kurudi katika nchi hizo mbili.

Kabuga mwenye umri wa miaka 88 alishutumiwa kueneza chuki kupitia kituo cha redio na televisheni cha RTLM, alishtakiwa mahakamani kwa kuwa rmuasisi wake, na kuchochea mauaji hayo, ambapo zaidi ya watu 800,000 waliuawa wakati wa mauaji ya kimbari ya siku 100 nchini Rwanda, kuanzia mwezi wa Aprili (4) mwaka 1994. Alikana mashtaka.

Chanzo: Bbc