Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

KCB Bank imekamilisha manunuzi ya hisa za BPR Bank ya Rwanda

Kcb 3 KCB Group imeinunua BPR Bank ya Rwanda

Thu, 26 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Benki ya KCB Group ya nchini Kenya, imekamilisha taratibu za kununua hisa za benki ya Banque Populaire du Rwanda (BPR) kutoka kwenye soko la hisa la Atlas Mara Mauritius and Arise.

Joshua Oigara, CEO wa KCB, amesema ununuzi huo umefanikiwa baada ya kufata taratibu zote za kimamlaka nchini Kenya, pamoja na kupewa baraka kutoka mamlaka za mikopo na mitaji nchini Rwanda hivyo kufanya KCB kuwa mmiliki mkubwa hisa za BPR, ambayo ni benki ya pili kwa ukubwa nchini Rwanda.

"Muungano huu wa BPR na KCB Group utatupeleka kwenye viwango vya juu sana, itatupa uwezo mkubwa na imara kwenye masuala ya kifedha pamoja na kuweza kusukuma gurudumu la kiuchumi kwa nchi za Afrika Masharikiā€¯ amesema Oigara kutokea Nairobi.

KCB inaendesha shughuli zake kwenye nchi za Tanzania, Sudan Kusini, Uganda, Rwanda, Burundi na pia ina matawi nchini Ethiopia.

CEO huyo ameongeza kuwa muungano huo sasa unakwenda kuunda benki moja ambayo itafanya shughuli zake nchini Rwanda na shughuli zote za BPR na KCB zitaendelea kama ilivyokuwa awali.

Oigara ameeleza pia mipango ya KCB kununua hisa kwa asilimia 100 kutoka African Banking Corporation tawi la Tanzania (BancABC), pia imenunua hisa asilimia 96.6 kutoka ABC Holdings pamoja na hisa asilimia 3.4 kutoka Tanzania Development Finance Company.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live