Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

KAGAME: 'Nipo tayari kwa lolote' mzozo wa DRC na Rwanda

Rwanda Kagame Paul Kagame, Rais wa Rwanda

Wed, 6 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Rwanda Paul Kagame anasema anatarajia mema lakini "amejitayarisha kwa mabaya zaidi" kuhusu mzozo kati ya nchi yake na nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

DR Congo inaishutumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa Congo wa M23 na hivi majuzi ilisitisha mikataba yote ya biashara na ushirikiano. Rwanda inakanusha madai hayo.

Rais Kagame anatarajiwa kufanya mazungumzo na mwenzake wa Congo, Rais Félix Tshisekedi siku ya Jumatano katika mji mkuu wa Angola, Luanda.

Mazungumzo hayo yanasimamiwa na Rais wa Angola João Lourenço.

Lakini kabla ya mkutano huo, Rais Kagame ametuma ujumbe katika mtandao wa twirtter akisema anajiandaa kwa mabaya zaidi.

"Natarajia mema kwa sisi sote, Congo na Rwanda. Lakini kama yaliyo bora hayatakuja, watakuta nimejiandaa kwa mabaya. Hiyo ndiyo njia ya kwanza ninayoishughulikia. Ninajiandaa kwa mabaya lakini ninawatakia mema zaidi na ninamaanisha."

Rais wa Rwanda anasema hakuna "suluhisho la kichawi" katika mvutano kati ya majirani hao wawili.

"Hakuna suluhisho la uchawi hapa kwangu zaidi ya kuwasilisha ukweli kama ninavyouelewa na ukweli umeshawasilishwa... sio watu kuunda ukweli wao wenyewe au kufikiria tu kwamba watatoa suluhisho kwa upande mmoja au mwingine."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live