Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jumuiya ya kimataifa yajipanga kutuma misaada Libya

Mafuriko Ya Libya: Mji Wa Derna Pekee Wapata Miili 1,000   Waziri Jumuiya ya kimataifa yajipanga kutuma misaada Libya

Wed, 13 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

dara ya huduma za dharura inajaribu kuhesabu idadi ya waathiriwa ktokana na kimbunga Daniel kilichopiga kwenye pwani ya mashariki ya Libya siku ya Jumapili. Mvua kubwa na kuporomoka kwa mabwawa mawili kulisababisha uharibifu mkubwa wa sehemu ya mji wa Derna, unaokaliwa na wakaazi100,000. Jumuiya ya kimataifa inajipanga kutoa msaada wa dharura.

Vitongoji vilimezwa na maji, mabwawa yalivunjika, maporomoko ya matope ambayo yalisomba majengo kadhaa. Hali ni mbaya nchini Libya, baada ya mafuriko yaliyosababishwa na kimbunga Daniel Jumapili ya wiki iliyopita mashariki mwa nchi hiyo.

Idara ya huduma za dharura nchini Libya ya serikali yenye makao yake mjini Tripoli, inayotambuliwa na jumuiya ya kimataifa, ilitoa idadi ya mwisho ya vifo vya watu Jumanne mchana. Kulingana na msemaji wa idara hiyo, Osama Ali, kimbunga Daniel kilisababisha vifo vya watu 2,300 na wengine 7,000 kujeruhiwa katika mji wa Derna pekee, ambao ni wazi kuwa ndio ulioathiriwa zaidi.

Serikali ya mashariki, pinzani kwa ile ya Tripoli imebaini kwamba idadi hiyo ni kubwa zaidi. Inadai kwamba watu zaidi ya 5,200 waliangamia katika tukio hilo. Hata hivyo waziri wa Afya anasema anatarajia idadi ya waathiriwa kuwa maradufu zaidi. Kwa hivyo idadi sahihi ya watu waliofariki haijulikani. Shirikisho la kimataifa la mashirika ya Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu linasalia kuwa angalifu kuhusu takwimu, lakini linatambua idadi "kubwa" ya vifo ambavyo vinaweza kuhesabiwa kwa maelfu. Shirikisho hilo linakadiria idadi ya waliotoweka kuwa 10,000. Pia kuna vifo vingine 65 katika miji mingine mashariki mwa Libya.

Afisa wa IFRC anazungumzia mahitaji ya kibinadamu ambayo yanazidi kwa mbali uwezo wa Shirikisho, na hata yale ya serikali.

Tunachoweza kusema ni kwamba watu elfu kadhaa walikufa. Maelfu kadhaa walipteza makazi yao na maelfu ya familia wamekwama chini ya vifusi au kutoweka. Timu za Shirika la Msalaba Mwekundu zilitumwa mara moja. Wanafanya wawezavyo lakini mahitaji ni makubwa sana. Yanazidi uwezo wa Shirika la Msalaba Mwekundu na hata uwezo wa mamlaka ya Libya

Uturuki yatuma waokoaji karibu mia moja

Kulingana na waokoaji, kadiri muda unavyopita, ndivyo uwezekano wa kupata manusura unavyopungua. Kwa kukabiliwa na hali hii ya dharura, nchi za kigeni zimetuma timu za waokoaji. Waokoaji kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu na Uturuki wamewasili eneo la tukio. Ankara ilituma waokoaji 168, magari mawili na boti mbili za uokoaji, mablanketi mia kadhaa, mahema na vifurushi, karibu jenereta ishirini. Uwasilishaji huu wa kwanza wa msaada wa kibinadamu wa Uturuki mashariki mwa Libya unaweza kuonekana kuwa mdogo kutokana na mahitaji makubwa, lakini ulikuwa wa haraka na unasisitiza uhusiano wa karibu kati ya nchi hizo mbili.

Rais Recep Tayyip Erdogan, ambaye aliagiza msaada huo kutumwa ndani ya ndege za jeshi la Uturuki, alizungumza kwa njia ya simu na mkuu wa Baraza la Rais wa Libya, Mohammed el-Menfi. Alimhakikishia kwamba msaada huu utaendelea, anaripoti mwandishi wetu wa Istanbul, Anne Andlauer.

Uturuki ni mshirika muhimu nchini Libya katika miaka ya hivi karibuni. Iliiunga mkono kijeshi Serikali ya Umoja wa Kitaifa (GNA) yenye makao yake makuu mjini Tripoli dhidi ya vikosi vya Jenerali Khalifa Haftar, kiongozi wa kivita mashariki mwa nchi hiyo. Wakati ikiendelea kuunga mkono mamlaka huko Tripoli, inayotambuliwa na jumuiya ya kimataifa, Ankara imeanzisha uhusiano na mashariki tangu mwaka jana, hata kupeleka juhudi za upatanishi katika nchi hii iliyogawanyika kati ya serikali mbili zinazokinzana. Serikali iliyoteuliwa na Baraza la Wawakilishi la Tobruk, upande wa mashariki, pia iliishukuru Uturuki kwa msaada wake baada ya maafa hayo. Ufaransa itajenga hospitali

Misri, Italia na Algeria pia zilitangaza kutumwa kwa misaada ya kibinadamu. Ufaransa itajenga hospitali ndani ya "saa 24 hadi 48", Élysée ilitangaza Jumanne hii, Septemba 12. "Rais wa Jamhuri ameamua kutuma timu za dharura kutoka kwa Usalama wa raia na kujenga hospitali ", yaani karibu "yaanzi raia na wanajeshi zaidi ya hamsini ambao wanaweza kutibu watu 500 kwa siku", ilibaini Ofisi ya Rais.

Kwa hivyo mvua hiyo kubwa ilisababisha kuporomoka kwa mabwawa mawili ambayo hayakutunzwa vizuri. Tukio hilo lilitokea usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu. Mbali na vitongoji vyote kuharibiwa, barabara na madaraja yamekatwa. Magari yalibebwa na maji hadi baharini.

Ni vigumu kuutambua tena mji wa Derna. Miili mingi inaonekana mjini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live