Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jumuia ya kimataifa yaombwa kutoa chanjo ya Monkeypox Afrika

Chanjo Ya Money Jumuia ya kimataifa yaombwa kutoa chanjo ya Monkeypox Afrika

Thu, 15 Sep 2022 Chanzo: VOA

Wakati visa vya maambukizi ya Monkeypox vikiendelea kushuka kwenye mataifa ya Ulaya pamoja na Marekani, wataalam wa sayansi wanasema kwamba sasa ni wakati wa kuweka kipaumbele cha upatikanaji wa chanjo dhidi ya maradhi hayo barani Afrika.

Wakati visa vya maambukizi ya Monkeypox vikiendelea kushuka kwenye mataifa ya Ulaya pamoja na Marekani, wataalam wa sayansi wanasema kwamba sasa ni wakati wa kuweka kipaumbele cha upatikanaji wa chanjo dhidi ya maradhi hayo barani Afrika.

Mwezi Julai, shirika la kimataifa la afya WHO liliorodhesha monkeypox kuwa dharura ya kimataifa, wakati likiomba jumuia ya kimataifa kusaidia mataifa ya kiafrika ili kuepuka ukosefu wa usawa wa chanjo, kama uliyoshuhudiwa wakati wa janga la Covid-19.

Hata hivyo macho ya ulimwengu hayakuelekezewa kwenye bara hilo, huku kukikosa taifa hata moja tajiri lililotoa chanjo kwa ajili ya Afrika, wakati wataalam wakionya kwamba hamu ya kusaidia bara hilo huenda ikadidimia kabisa.

Placide Mbala ambaye ni mtafiti wa magonjwa ya virusi kutoka taasisi ya kimatibabu ya Congo amesema kwamba hakuna lililobadilika kwa kuwa ulimwengu unashugulikia maambukizi ya monkeypox kwenye mataifa ya magharibi.

Ameongeza kusema kwamba mataifa ya kiafrika ambako ugonjwa huo imekuwa kwa muda mrefu yamekuwa dhaifu ifikapo kwenye masuala ya utafiti, ufuatiliaji, upimaji pamoja na matibabu kwa wagonjwa.

Monkeypox umeambukiza watu kwenye baadhi ya maeneo ya magharibi na kati mwa Afrika tangu miaka ya 70, lakini ulianza kuzungumziwa kwa kina baada ya kuzuka barani Ulaya na Marekani hivi karibuni, wataalam wa afya wakipendekeza kwa mara ya kwanza kutumika kwa chanjo dhidi yake.

WHO imesema kwamba itaweka mikakati ya ugawaji wa chanjo ili kuhakikisha mataifa maskini yanazipata pia.

Chanzo: VOA