Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jumba aliloishi Mandela hadi kifo latelekezwa

Jumba Aliloishi Mandela Hadi Kifo Latelekezwa Jumba aliloishi Mandela hadi kifo latelekezwa

Mon, 11 Dec 2023 Chanzo: Radio Jambo

Ikiwa ni miaka 10 baada ya kifo cha rais wa kwanza wa Afrika Kusini huru ambaye pia alisifiwa kama shujaa wa kupinga ubaguzi wa rangi Nelson Madiba Mandela, imebainika kwamba jumba la kifahari aliloishi hadi pumzi yake ya mwisho sasa limesalia kuwa mahame chakavu tu yenye magofu.

Kwa mujibu wa shirika la habari la ENCA nchini Afrika Kusini ambalo hivi karibuni lilifanya ziara katika boma hilo lililoko katika mtaa wa kifahari uitwao Houghton, walibaini picha za kukatisha tamaa kwani jumba hilo limebaki kuwa magofu tu yasiyovutia.

Boma la kifahari la Houghton linatajwa kuwa moja ya sehemu za mwisho kabisa alizoziita nyumbani na huko ndiko alitembelewa na watu wenye haiba iliyotukuka wakiwemo aliyekuwa mke wa rais wa Marekani, Michelle Obama, msanii wa Soul Michael Jackson, mwanahabari Oprah Winfrey miongoni mwa wengine.

“Kwa kumkumbuka mtu tunayejivunia kumwita 'Baba wa Taifa letu', tunaangalia jinsi nyumba hii inavyoendelea kwa sasa,” ENCA walisema wakati wa ziara katika boma hilo chakavu.

Chombo hicho cha habari kinashiriki kwamba sababu inayofanya nyumba hii kusimama bila watu na kutelekezwa ni kwa sababu ya mizozo ya kifamilia.

Waliripoti kwamba wosia wa Mandela ulisema kwamba watoto wake wanaweza kuishi nyumbani bila kupangishwa kwa kulipa kodi.

Chanzo: Radio Jambo