Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jumanne, Septemba 14: Watu 451 waambukizwa COVID-19 Kenya

23c099d0962064cf Jumanne, Septemba 14: Watu 451 waambukizwa COVID-19 Kenya

Tue, 14 Sep 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Wizara ya Afya imeripoti visa vipya 451 vya coronavirus kutokana na sampuli ya 6,833 zilizopimwa katika saa 24 zilizopita.

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe alisema Jumanne, Septemba katika taarifa kwamba kiwango cha chanya kwa sasa ni asilimia 6.6.

Alidokeza kuwa kutokana na visa hivyo vipya wagonjwa 436 ni Wakenya nao 15 ni raia wa kigeni akiongeza kwamba wagonjwa 244 ni wanawake nao 207 ni wanaume

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe alisema Jumanne, Septemba katika taarifa kwamba kiwango cha chanya kwa sasa ni asilimia 6.6.

Alidokeza kuwa kutokana na visa hivyo vipya wagonjwa 436 ni Wakenya nao 15 ni raia wa kigeni akiongeza kwamba wagonjwa 244 ni wanawake nao 207 ni wanaume.

Mgonjwa mwenye umri wa chini ni mtoto wa miezi miwili naye mkongwe ana miaka 95.

Jumla ya visa vilivyothibitishwa nchini Kenya sasa vimefika 244,380, na jumla ya sampuli zilipomwa tangu mwezi Machi nazo zikigonga 2,464,459.



Kagwe alisema kuwa wagonjwa 835 wamepata nafuu, 770 kati yao walikuwa wakihudumiwa makwao nao 65 wakipata matibabu katika vituo mbali mbali vya afya nchini.

Jumla ya waliopona sasa ni 234,737.

Wakati uo huo, wagonjwa 5 wameripotiwa kupoteza maisha yao kutokana na makali ya ugonjwa huo.

Jumla ya wagonjwa walioangamizwa kutokana na makali ya maradhi hayo Kenya imetimia 4,7928.

Aidha wagonjwa 1,559 kwa sasa wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya nchini kote nao 3,427 wanahudumiwa manyumbani mwao.

Aidha wagonjwa 122 wamelazwa katika ICU.

Maambukizi mapya katika kaunti ni kama ifuatavyo;

Nairobi 115, Nakuru 67, Uasin Gishu 28, Kiambu 26, Nyandarua 21, Garissa 21, Murang’a 20, Migori 18, Meru 15, Baringo 10, Laikipia 10, Kitui 10, Machakos 9, Narok 8, Kakamega 7, Turkana 7, Marsabit 6, Mombasa 6, Nandi 6, Elgeyo Marakwet 6, Kajiado 6, Kisumu 5, Bungoma 4, Busia 4, Kilifi 4, Nyeri 4, Bomet 2, Makueni 2, and Tharaka Nithi 1, Kisii 1, Lamu 1 and Nyamira 1.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke