Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Julius Malema: Tutamlinda Putin dhidi ya ICC

Malema Putin.jpeg Julius Malema na Putin

Fri, 24 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama cha wachache cha upinzani cha Afrika Kusini, Economic Freedom Fighters (EFF), kimesema Rais wa Urusi Vladimir Putin anakaribishwa kuzuru Pretoria licha ya hati ya kukamatwa iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) dhidi yake.

Mahakama ya ICC, ambayo Afrika Kusini imetia saini, imemshutumu Putin kwa uhalifu wa kivita, ambao ni pamoja na utekaji nyara wa watoto wa Ukraine katika uvamizi unaoendelea wa Urusi nchini Ukraine.

Bw Putin ameratibiwa kwenda Afrika Kusini kwa mkutano wa kilele wa Brics (Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini) mwezi Agosti.

Kiongozi wa EFF Julius Malema siku ya Alhamisi alisema hakuna mtu atakayemkamata Bw Putin akiwa Afrika Kusini, nchi ambayo Urusi “ilichukua jukumu kubwa la kuunga mkono mapambano ya uhuru”.

Malema alisema kuwa serikali ya Afrika Kusini haipaswi kukubali shinikizo kutoka kwa ICC, ambayo aliishutumu kwa “unafiki”.

“Putin anakaribishwa hapa. Hakuna atakayemkamata Putin. Ikibidi tutaenda kumchukua Putin kutoka uwanja wa ndege hadi kwenye mikutano yake. Atahutubia, atamaliza mikutano yake yote, na tutamrudisha uwanja wa ndege, “Bwana Malema alisema.

“Tunawajua marafiki zetu. Tunawajua watu waliotukomboa. Tunawajua watu waliotuunga mkono,” aliongeza.

Afrika Kusini ina uhusiano wa karibu wa kidiplomasia na Moscow licha ya kulaaniwa na nchi za Magharibi. Mwezi uliopita, jeshi lake la wanamaji lilifanya mazoezi ya pamoja na vikosi vya Urusi katika pwani ya Afrika Kusini. Pia imejizuia wakati wa kura za Umoja wa Mataifa kulaani uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Mnamo mwaka wa 2015, serikali ya Afrika Kusini ilikosolewa kwa kumruhusu Rais wa Sudan Omar al-Bashir kuondoka nchini licha ya kibali cha kukamatwa kwa ICC.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: