Vikosi vya uokoaji nchini Sudan vinaendelea na jitihada za kuinasua miili ya wachimbaji wa madini waliofukiwa katika mgodi wa dhahabu uliopo Jimbo la Kordofan, Magharibi mwa nchi hiyo.
Mkurugenzi wa mgodi ilipotokea ajali hiyo ambao unamilikiwa na serikali ya nchi hiyo, Khaled Al Dahwey ameliambia Shirika la Habari la CNN kwamba watu 36 walikuwepo ndani ya mgodi huo wakati ajali ikiyokea ambapo ni mtu mmoja pekee ndiye aliyenusurika.
Jitihada za uokoaji zimeendelea kwa siku kadhaa tangu ajali hiyo ilipotokea, Jumapili ya Desemba 26 ambapo kazi imekuwa ngumu kutokana na kina kirefu cha mgodi huo, kinachofikia umbali wa mita 20 kwenda chini.