Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jubilee wamtaka Naibu Rais Ruto kuonesha nyaraka za ulipaji kodi

Tuju2 Katibu Mkuu wa Chama cha Jubilee, Raphael Tuju

Tue, 7 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu wa Chama cha siasa cha Jubilee nchini Kenya, amemtaka Naibu wa Rais Willima Ruto, kuonesha risiti za malipo ya Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato KRA nchini humo,kuhusu biashara yake ya ufugaji wa kuku.

Katibu Huyo ametoa kauli hiyo kufuatia ushahidi wa maneno aliyotoa Naibu Rais alipokuwa akijinadi kuwa anaingia takribani Shilingi milioni 1.5 za nchini humo kila siku kutokana na biashara hiyo.

"tunampongeza snaa Naibu wa Rais kwa biashara yake ya ufugaji kuku inayomuingizia Milioni 1.5 kila siku, pia tunamuomba atuoneshe risti za malipo ya Kodi kutoka KRA, Mpeni kaisali yalioyo yake Kaisali"amesema katibu huyo.

Hata hivyo amewataka wananchi waliokuwa wakiendesha michango ya kumchangia kiongozi huyo kuacha mara moja kwani kwa aina ya biashara anayofanya anaweza kumudu gharama zote peke yake

Chanzo: www.tanzaniaweb.live