Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jubilee kuwasilisha kesi kortini kupinga matokeo ya uchaguzi mdogo wa Kiambaa

20801114330e2fe0 Jubilee kuwasilisha kesi kortini kupinga matokeo ya uchaguzi mdogo wa Kiambaa

Tue, 20 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Jubilee kimelaumu Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kwa ushinde huo wa Alhamisi, Julai 15, kikitaka kura hizo zihesabiwe upyaNaibu mwenyekiti wa Jubilee David Murathe pia alishtumu IEBC kwa kukataa kuhesabu kura upya licha ya mwaniaji wao Kariri Njama kupinga baadhi ya matokeo Njama alisisitiza kuwa ndiye mshindi wa uchaguzi huo mdogo na hawezi kubali kushindwa

Chama tawala cha Jubilee kimesema kitawasilisha kesi kortini kupinga matokeo ya uchaguzi mdogo wa kiti cha ubunge Kiambaa ambapo chama cha United Democratic Alliance (UDA) kilitwaa ushindi.

Jubilee kimelaumu Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kwa ushinde huo wa Alhamisi, Julai 15, kikitaka kura hizo zihesabiwe upya.

Kulingana na chama hicho, IEBC haikufuata sheria wakati wa kuendesha uchaguzi huo.



Read also

Magazeti Jumatatu, Julai 19: Kijiji Chapoteza Watu 13 Katika Mkasa wa Siaya

Mkutano wa dharuraHatua hii ni kufuatia mkutano ulioandaliwa Jumatatu, Julai 19, Kamati ya Kitaifa ya Usimamizi (NMC) Jubilee, ilipokutana na viongozi wa chama hicho walioendesha kampeni za Kiambaa.

Mkutano huo uliandaliwa katika Makao Makuu ya Jubilee, eneo la Pangani jijini Nairobi.

"Hatujaridhishwa na namna IEBC iliendesha uchaguzi huo, haswa wakati wa kujumilisha matokeo, tunataka kura zihesabiwe upya," ilisoma taarifa ya Jubilee.

Naibu mwenyekiti wa Jubilee David Murathe pia alishtumu IEBC kwa kukataa kuhesabu kura upya licha ya mwaniaji wao Kariri Njama kupinga baadhi ya matokeo.

Kariri Njama ajitawaza mshindiKwa upande wake Njama, alisisitiza kuwa ndiye mshindi wa uchaguzi huo mdogo na hawezi kubali kushindwa.

"Ninasema hapa kwa ujasiri kwamba nilishinda. Nawahakikishia watu wetu kuwa nitapigana hadi ushindi wa watu wa Kiambaa na kaunti ya Kiambu urejeshwe. Nitaendelea kuwatumikia."

"Nitaendelea kusimama na Rais Kenyatta. Kukitokea uchaguzi mwingine nitawania na tikiti ya chama cha Jubilee kwani ndio chaguo la watu wangu," alisema Njama.



Read also

Waruguru Adokezea Kurejea Tangatanga Baada ya Jubilee Kulambishwa Sakafu Kiambaa

Uchaguzi mdogo wa Kiambaa na Juja ndio umewapa kibaridi wandani wa Rais Uhuru Kenyatta wakihofia huenda wafuasi wa Mt Kenya watawahepa kisiasa.

Tayari wabunge kama Kanini Kega na Ngunjiri Wambugu walijitokeza na kusema katibu wa Jubilee Raphael Tuju na David Murathe wanafaa kuondoka kwenye uongozi wa chama.

Katika uchaguzi huo wa Alhamisi, Julai 15, mgombea wa UDA John Njuguna Wanjiku aliibuka mshindi kwa kujizolea kura 21773 huku mpinzani wake Kariri Njama wa Jubilee akipata kura 21263.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke