Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jubilee Kuondoa mkono wa Ruto kwenye nembo yake ili kumuaga

76a5c17882cf6528 Jubilee Kuondoa mkono wa Ruto kwenye nembo yake ili kumuaga

Sun, 4 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Kutuny alisema Ruto aliamua kuingia UDA na kwa hivyo wanataka kumuaga kabisa kutoka JubileeChama hicho kinaweka mikakati ya kupata sura mpya ili kisiwe na uhusiano wowote na DPMojawapo wa mikakati ni kuondoa mkono wa DP kutoka nembo yake na pia kubadilisha rangi zakeChama cha Jubilee kinapanga kuondoa mkono wa Naibu Rais William Ruto kwenye nembo yake katika harakati za mwisho kumuaga akiondoka.

Nembo ya Jubilee iliundwa na salamu za DP na Rais Uhuru Kenyatta wakati wa kuvunjwa kwa vyama vilivyounda Jubilee.

Kulingana na wandani wa Rais waliozungumza na gazeti la Nation Jumapili Julai 4, DP amekuwa mtundu na mkaidi chamani na sasa wanataka aondoke kabisa.

Wanasema amekuwa akipigia debe sera za chama cha United Democratic Alliance (UDA) na hivyo ni mshindani wa Jubilee.



Walisema Jubilee inapanga kumaliza uhusiano wake kabisa na DP na hivyo ni lazima wakipe chama sura mpya.

Katika kufanya hivyo, walisema rangi za chama hicho zitabadilishwa ili kuondoa zile zinazohusishwa na DP za majono na nyeusi.

"Rangi hizo zinaaminika kuwa mizizi ya DP katika chama kwani zilikuwa za chama chake kilichovunjwa cha URP. Nyekundu nayo huhusishwa na chama cha TNA kilichokuwa cha Rais Uhuru," mwandani wa Rais aliambia TUKO.co.ke

Kando na rangi, nembo ya chama hicho mabayo huwa ni mikono inayosalimiana huhusishwa na DP na Uhuru.

Nembo hiyo ilitokana na sakamu zao za kuleta vyama vyote pamoja ili kuunga Jubilee ambayo walitumia kuingia Ikulu kwa kipindi cha pili.

Naibu katibu wa chama Joshua Kutuny alisema tayari viongozi wamefanya mkutano jijini na kuafikiana hilo na kwa sasa kinachosalia ni wanachama wote wa Jubilee kukutana na kuidhinisha hilo.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke