Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Joy kortini akidaiwa kuiba Range Rover ya bosi wake

BYUgC3aH.jpeg Joy kortini akidaiwa kuiba Range Rover ya bosi wake

Mon, 25 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamke mmoja mkazi wa jijini Nairobi nchini Kenya, amepandishwa kizimbani kwa tuhuma za wizi wa gari la mwajiri wake.

Mwanamke huyo aitwaye Joy Kaaria ameshtakiwa kwa kosa la kuiba gari hiyo aina ya Range Rover Evoque, yenye thamani ya Ksh3.2 milioni sawa na Sh52 milioni za Tanzania.

Mbele ya Hakimu Mkuu Mwandamizi wa Mahakama ya Milimani, Dolphine Alego, Joy alikana kuiba gari hilo Jumamosi Septemba 30, katika Kituo cha Biashara cha Crescent.

Tovuti ya Tuko ya nchini humo, imemtaja mwajiri anayedaiwa kuibiwa gari kuwa ni kampuni ya Revere Technologies Limited.

Wakili anayemtetea Joy, ameomba masharti nafuu ya dhamana akisisitiza kuwa mtoto mdogo wa mteja wake ameachwa nyumbani peke yake, huku akiwa na kiwewe.

Wakili huyo ameieleza mahakama kwamba Joy aliachishwa kazi Septemba na bado hajalipwa stahili zake.

"Mteja wangu alifukuzwa kazi tangu Septemba 2023 na hakuwahi kulipwa stahiki zake na kwa hivyo naomba mahakama hii iwe na utulivu katika kuamua dhamana yake," alisema wakili huyo

Chanzo: www.tanzaniaweb.live