Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jinsi uvamizi wa Urusi nchini Ukraine unavyoathiri usambazaji wa chakula barani Afrika

Wheat Jinsi uvamizi wa Urusi nchini Ukraine unavyoathiri usambazaji wa chakula barani Afrika

Fri, 25 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ngano na nafaka nyingine zimerejea katika kiini cha siasa za kijiografia kufuatia uvamizi wa Urusi nchini Ukraine. Nchi zote mbili zina jukumu kubwa katika soko la kimataifa la kilimo.

Kuna biashara kubwa ya kilimo kati ya nchi za bara na Urusi na Ukraine. Nchi za Afŕika ziliagiza bidhaa za kilimo zenye thamani ya dola bilioni 4 kutoka Russia mwaka 2020. Takriban asilimia 90 ya hii ilikuwa ngano, na asilimia sita ilikuwa mafuta ya alizeti.

Nchi kuu zilizoagiza kutoka nje zilikuwa Misri, ambayo ilichangia karibu nusu ya uagizaji, ikifuatiwa na Sudan, Nigeria, Tanzania, Algeria, Kenya na Afrika Kusini.

Vile vile, Ukraine ilisafirisha bidhaa za kilimo zenye thamani ya dola bilioni 2.9 kwa bara la Afrika mwaka 2020. Takriban asilimia 48 ya bidhaa hizo ni ngano, asilimia 31 ya mahindi, na iliyosalia ni pamoja na mafuta ya alizeti, shayiri na soya.

Urusi na Ukraine wana mchango mkubwa katika soko la kimataifa la bidhaa. Urusi inazalisha takriban asilimia 10 ya ngano duniani huku Ukraine ikiwa na asilimia nne. Ikiunganishwa, hii ni karibu saizi ya jumla ya uzalishaji wa ngano wa Umoja wa Ulaya. Ngano ni kwa matumizi ya ndani na pia masoko ya nje.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live