Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jinsi mwenye nyumba alivyo ’muua’ mtoto wa mpangaji

Jinsi Mwenye Nyumba Alivyoua Jinsi mwenye nyumba alivyo ’muua’ mtoto wa mpangaji

Mon, 8 May 2023 Chanzo: Bbc

Polisi katika jimbo la Ashanti nchini Ghana wameanza uchunguzi kuhusiana na tukio ambapo mwenye nyumba anashutumiwa kwa kumuua watoto wa mpangaji wake.

Katika tukio hilo, mpangaji na binti yake mwingine mwenye umri wa miaka 17 waliachwa na majeruhi makubwa na sasa wamelazwa katika hospitali kuu ya Ashanti- Ashanti General Hospital,huku hali yao ikiwa mahututi kutokana na majeruhi.

Maafisa wa polisi wanasema mshukiwa tayari amekamatwa na uchunguzi unaendelea kuhusiana na tukio hilo.

Tukio hili lililotokea siku ya Ijumaa baada ya malumbano kati ya kijana wa mwenye nyumba na baadhi ya wapangaji wake, baada ya mtoto wa mwenye nyumba kudaiwa kuwazuia wapangaji kuingia ndani ya vyumba wanavyopangisha, kwa kile alichosema kuwa kodi yao imeisha.

Taarifa za vyombo vya habari nchini Ghana zinasema kuwa, mke wa mpangaji aliyepigwa upanga alikuwa amelewa chakali wakati wa tukio hilo.

Chanzo: Bbc