Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jimbo la Niger lahaha kunusuru wanafunzi 130 waliotekwa

F80a27b7a61ebf93f0bce2654a1d8ad4.jpeg Jimbo la Niger lahaha kunusuru wanafunzi 130 waliotekwa

Sat, 5 Jun 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

UONGOZI wa Jimbo la Niger nchini Nigeria umesena unazungumza na watu wenye silaha waliowateka watoto wa shule zaidi ya 130 wiki iliyopita katika Shule ya Kiislamu ya Salihu Tanko.

Mkuu wa Shule hiyo, Abubakar Alhassan alizungumza na vyombo vya habari na kuiomba serikali ya Nigeria kufanya kila linalowezekana kuwaokoa watoto hao.

Mapema wiki, hii watu wenye silaha waliwateka watoto, katika shule moja ya Kiislamu katika Jimbo la Niger, ikiwa ni mwendelezo wa visa vya kutekwa kwa watoto nchini humo.

Msemaji wa polisi katika Jimbo la Niger, Wasiu Abiodun, alisema watekaji hao waliwasili katika shule hiyo iliyo kwenye mji wa Tegina wakiwa kwenye pikipiki na kuanza kufyatua risasi hewani kabla ya kutekeleza utekaji huo.

Taarifa mbalimbali nchini humo zinasema wanafunzi 200 ndio waliokuwa katika shule hiyo ya Kiislamu ya Tanko na haijafahamika ni watoto wangapi walitekwa na wapi wamepelekwa.

Hata hivyo, afisa wa shule hiyo alisema watoto waliotekwa ni zaidi ya 100 lakini waliokuwa wana umri wa kati ya miaka minne hadi 12 walirudishwa shuleni na watekaji hao.

Makundi yenye silaya yameendelea kuleta taharuki Kaskazini Magharibi na eneo la Kati nchini humo kwa kutekeleza utekaji kama huo ikiwa ni pamoja na kuiba mifugo.

Tangu Disemba mwaka 2020 watu wenye silaha wamewateka watoto na wanafunzi zaidi ya 730 hadi sasa nchini humo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz