Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jeshi lilofanya mapinduzi Guinea limetangaza kuunda serikali ya mpito

Mamady Doumbouya1 Mamady Doumbouya, Kiongozi wa Jeshi nchini Guinea

Tue, 7 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi lililofanya mapinduzi nchini Guniea limesema kuwa litaunda Serikali ya Mpito ya pamoja itakayo weza kusimamia nchi hiyo katika kipindi hiki ambacho wamemuondoa madarakani Rais Alpha Conde.

Wakiongozwa na Luteni Mkuu, Mamady Doumbouya, wamesisistiza kuwa hakutakuwa na machafuko wala umwagikaji wa damu katika kipindi hiki.

"Tutazindua mjadala wa mapendekezo ili kuona jinsi gani tunaeza kuweka vigezo vitakavyokuwa sawa katika kipindi hiki cha mpito, ili kuuda serikali ya mpito itakayotuvusha katika kipindi hiki" - Luteni Mamady.

Wanajeshi hao walifanya mapinduzi ya kumuoindoa Rais huyo, septemba 05, mwaka 2021, kwa madai ya kukithiri kwa vitendo vyarushwa, uonevu na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live