Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jeshi lililomuondoa Rais wa Guiner limeagiza Baraza la Mawaziri kuhudhuria mkutano leo

Guinea2 Wanajeshi waliofanya Mapinduzi Guinea, watoa amri kwa Baraza la Mawaziri Kukutana

Mon, 6 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikundi cha wanajeshi waliomwondoa Rais wa Guinea Alpha Condé mamlakani September 5, 2021 wameamuru baraza la mawaziri la nchi hiyo kuhudhuria mkutano wa lazima Jumatatu.

Taarifa hii imetolewa kupitia televisheni ya Taifa nchini humo, na kusistiza kuwa wale ambao watakataa kuhudhuria mkutano huo watachukuliwa kuwa waasi, taarifa kwenye Televisheni ya serikali imesema.

Hata hivyo, Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, na shirika la kikanda la Ecowas wamelaani mapinduzi hayo na kutoa wito wa kurejeshwa kwa utawala wa raia.

Mkuu wa vikosi maalum vya nchi hiyo, Kanali Mamady Doumbouya, amesema wanajeshi wake wamechukua madaraka kwa sababu wanataka kumaliza ufisadi uliokithiri na usimamizi mbaya

Chanzo: www.tanzaniaweb.live