Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jeshi lawashikilia waasi wa M23 kwa kuua raia 50

Jeshi Njeshi M23 DRC yawashikilia waasi wa M23 kwa kuua raia 50

Fri, 2 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Kongo limewashutumu waasi wa M23 kwa kuwaua takriban raia 50 katika mji wa mashariki wa Kishishe.

Haya yanajiri huku kukiwa na taarifa za mauaji ya watu wengi kufuatia kuanza tena kwa mapigano, huku usitishaji mapigano uliokubaliwa wiki iliyopita ukionekana kuporomoka.

Kundi hilo la waasi limekanusha madai dhidi yao kuwa "hazina msingi", likisema kuwa halijawahi kuwalenga raia

Maelfu ya watu wanakimbia mapigano kati ya waasi, vikosi vya serikali na wanamgambo washirika katika maeneo tofauti ya jimbo la Kivu Kaskazini.

Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zilikubaliana katika mazungumzo nchini Angola kwamba usitishaji vita utaanza kutekelezwa Ijumaa iliyopita.

M23 walisema mapatano hayo hayakuwahusu kwani hawakualikwa kwenye mazungumzo hayo. Rwanda inakanusha madai kwamba inaunga mkono M23

Chanzo: www.tanzaniaweb.live