Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jeshi lapigana na wanamgambo wa Amhara

Jeshi Mgamboooo Jeshi lapigana na wanamgambo wa Amhara

Thu, 3 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

jeshi la Ethiopia limepigana na watu wenye silaha wa kundi la wanamgambo wa eneo la Amhara, katika mzozo mpya kati ya pande mbili ambazo zilikuwa washirika katika mapigano ya miaka miwili kwenye eneo la Tigray.

Daktari katika hospitali moja ya mji wa Debre Tabor huko Amhara amesema watu wenye silaha kutoka Fano wamepigana na Jeshi la Taifa la Ulinzi la Ethiopia karibu na mji huo, Jumanne na Jumatano ya jana.

Ameongeza kuwa hospitali hiyo imepokea watu kadhaa wenye majeraha mabaya, yakiwemo majeraha ya risasi na silaha nzito.

Wakazi wa eneo la Kobo wamesema mapigano makali yalizuka pia nje ya mji huo mapema Jumanne asubuhi, lakini yalitulia kiasi jana Jumatano.

Ni vyema kutambua kwamba, wanamgambo wa Fano wanafanya shughuli zao bila ya muundo maalumu wa uongozi, na waliunga mkono kampeni ya vikosi vya jeshi la Shirikisho katika vita vya miaka miwili eneo jirani la Tigray, vilivyomalizika Novemba mwaka jana.

Uhusiano wa pande hizo mbili umedorora kutokana na kile ambacho baadhi ya watu katika eneo hilo wanasema ni serikali ya Ethiopia kupuuza masuala ya usalama katika eneo la Amhara.

Kwa upande mwingine, chanzo cha kidiplomasia kimesema kuwa mapigano hayo yalianza siku kadhaa zilizopita, wakati jeshi la taifa lilipoanzisha operesheni ya kuwalazimisha wanamgambo wa Fano kuondoka Kobo na maeneo mengine

Chanzo: www.tanzaniaweb.live