Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jeshi lamuachia Waziri Mkuu Sudan

Fde71663d179d2219279e98e48869297 Jeshi lamuachia Waziri Mkuu Sudan

Wed, 27 Oct 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Waziri Mkuu wa Sudan, Abdalla Hamdok ameachiwa na kurudi nyumbani kwake baada ya siku kadhaa kuwekwa chini ya ulinzi na jeshi la nchi hiyo kwa kile kinachodhaniwa kuwa ni jaribio kupindua utawala wa nchi hiyo.

Taarifa ilyotolewa na ofisi ya Hamdok ilisema waziri huyu aliachiwa na mke wake hata hivyo baadhi ya viongozi na maafisa wengine wa kiraia walisalia kizuizini.

Miongoni mwa viongozi waliopaza sauti zao kutaka kuachiwa kwa kiongozi huyo ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron huku wakiyataka mataifa yenye nguvu duniani kuungana kupinga vitendo hivyo.

Jana baadhi ya waandamanaji wanaounga mkono demokrasia walirejea barabarani, wakifunga barabara katika mji mkuu kwa kuweka vizuizi vya muda na kuchoma matairi.

Aidha, wanajeshi waliwawafyatulia baadhi ya waandamanaji na kuuwa raia wanne kwa mujibu wa ripoti ya madaktari.

Chanzo: www.habarileo.co.tz