Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jeshi la Wanamaji la Morocco laokoa wahamiaji haramu 56

Lampedusa: Mtoto Mchanga Afariki Kwenye Boti Ya Wahamiaji Ya Italia Jeshi la Wanamaji la Morocco laokoa wahamiaji haramu 56

Tue, 28 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la wanamaji la Morocco lilitangaza jana kwamba limefanikiwa kuokoa wahamiaji haramu 56 waliokuwa wamejirundika kwenye mashua moja dhaifu nje ya pwani ya Atlantiki.

Shirika rasmi la habari la Morocco MAP limetangaza habari hiyo Jumatatu na kuongeza kuwa meli ya doria ya jeshi la wanamaji la Morocco iliizuia mashua hiyo juzi Jumapili wakati wa operesheni ya kutoa msaada karibu na bandari ya Tan-Tan.

Shirika hilo la habari limemnukuu afisa mmoja wa jeshi la Morocco akithibitisha habari hiyo ingawa hakutaka kutajwa jina lake na kuongeza kuwa, watu waliookolewa, ni pamoja na raia 55 wa nchi za Afrika za kusini mwa Jangwa la Sahara na mmoja ni raia wa Cuba. Walikuwa wako njiani kuelekea Visiwa vya Canary nchini Uhispania. Juhudi za kuzuia uhamiaji haramu

Vilevile amesema: Baada ya kupokea huduma muhimu, wahamiaji hao waliookolewa wamekabidhiwa kwa "Royal Gendarmerie" kikosi maalumu cha ufalme wa Morocco katika bandari ya Tan-Tan kwa ajili ya taratibu za kawaida za kiutawala.

Vyombo vya habari vilivyoripoti habari hiyo vimeongeza kuwa, hatua hiyo inafuatia operesheni nyingine kama hiyo iliyofanywa na Jeshi la Wanamaji la Kifalme la Morocco ambayo ilipelekea kuokolewa wahamiaji 47 raia wa nchi za Afrika za kusini mwa Jangwa la Sahara karibu na mji wa Dakhla.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, operesheni hizo ni sehemu ya mfululizo wa juhudi za uokoaji zinazofanywa na Jeshi la Wanamaji la Morocco, ikiwa ni pamoja na uokoaji wa nyakati tofauti wa wahamiaji 62 na 274 karibu na mji wa Dakhla, pamoja na kuokolewa wahamiaji 189 wa Senegal.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live