Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jeshi la Uganda limekanusha kumtesa mwanaharakati wa upinzani

Jeshi La Uganda Limekanusha Kumtesa Mwanaharakati Wa Upinzani Jeshi la Uganda limekanusha kumtesa mwanaharakati wa upinzani

Wed, 15 Feb 2023 Chanzo: Bbc

Jeshi la Uganda limekanusha tuhuma za kumteka nyara na kumtesa mwanaharakati wa upinzani, siku moja baada ya picha kuibuka zikimuonesha mwathiriwa akiwa na alama za mateso zinazoonekana kifuani mwake.

Katika msururu wa jumbe za Twitter, kiongozi wa upinzani Bobi Wine alikuwa amesema mfuasi wake alichomwa na kifaa cha chuma kilichotiwa moto kifuani na vyuma vilitumika kurarua ngozi yake.

"Hii imekuwa hatima ya mamia ya wafuasi wetu wanaotekwa nyara mara kwa mara!"alisema.

Lakini msemaji wa jeshi alisema uchunguzi wa ndani uligundua kuwa mwathiriwa, Eric Mwesigwa, "hakuwa mikononi mwa chombo chochote cha usalama".

"Tunamshauri aende kwa Tume ya Haki za Kibinadamu ya Uganda (UHRC) na kuripoti au polisi ili tuanze uchunguzi wa kina," msemaji huyo aliongeza.

Chanzo: Bbc