Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jeshi la Uganda laua waasi wa ADF wanaohusishwa na mauaji ya watalii

 ADF Jeshiiiiiiiiiiiiii Jeshi la Uganda laua waasi wa ADF wanaohusishwa na mauaji ya watalii

Fri, 3 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Uganda limetangaza leo Alkhamisi kuwa limeua waasi sita wa Allied Democratic Forces (ADF) na kumkamata kamanda anayeaminika kuhusika na mauaji ya watalii wawili wa kigeni na mwongozaji wao raia wa Uganda katika mbuga ya wanyama ya magharibi mwa nchi hiyo iliyoko karibu na mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrsia ya Kongo (DRC).

Dick Olum, kamanda mkuu wa kikosi cha pamoja cha Uganda na DRC cha kupambana na waasi wa ADF amesema kwenye taarifa yake hiyo kwamba, waasi hao waliuawa wakati wa mapigano makali kando ya Ziwa Edward ambalo linaainisha mpaka wa Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mapigano hayo yalitokea Jumanne usiku.

Aidha amesema: "Wanne kati ya waasi hao walikufa maji ziwani wakati wakijaribu kukimbia, huku wawili wakipigwa risasi na kujeruhiwa vibaya. Walijaribu kunusuru maisha yao kwa kuogelea kuvuka mto lakini hawakuweza kufika mbali bali walikufa maji."

Amesema: “Tulipata vitu kadhaa vinavyohusiana na tukio lililohusisha mauaji ya watalii hao wawili, ikiwa ni pamoja na vitambulisho vya taifa vya watalii waliouawa.” waasi wa ADF

Watalii hao walikuwa ni wanandoa wa kigeni waliokuwa kwenye fungate na ambao walijulikana kwa majina ya David na Cecilia Barlow, na mwongozaji wao raia wa Uganda aliyejulikana kwa jina la Eric Alyai. Waliuawa wakati gari lao la liliposhambuliwa katika Mbuga ya Taifa ya wilaya ya Kasese ya magharibi mwa Uganda Oktoba 17, 2023.

Tarehe 18 Oktoba, serikali ya Uganda kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (UWA) iliwahakikishia watalii usalama wao kufuatia shambulio la kigaidi la Jumanne jioni lililopelekea watalii wawili wa kigeni na mwongozaji wao mmoja raia wa Uganda kuuawa karibu na Mbuga ya Kitaifa ya magharibi mwa nchi hiyo.

Kwenye taarifa yake, Mamlaka ya Usimamiaji wa Wanyamapori nchini Uganda (UWA) ilisema: "Watu wasiojulikana" walivamia gari la watalii hao na kulichoma moto kwenye eneo la Nyamunuka, kando ya Barabara ya Katwe inayoelekea kwenye mbuga hiyo ya taifa ya magharibi mwa Uganda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live