Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jeshi la Uganda lamkamata kamanda wa kundi la waasi wa ADF

Jeshi La Uganda Lamkamata Kamanda Wa Kundi La Waasi Wa ADF Jeshi la Uganda lamkamata kamanda wa kundi la waasi wa ADF

Sun, 19 May 2024 Chanzo: Bbc

Jeshi la Uganda limemkamata kamanda wa kundi la waasi linaloshirikiana na Islamic State ambaye ni mtaalamu wa kutengeneza vilipuzi, au mabomu, ambayo kundi hilo limetumia kufanya mashambulizi mabaya siku za nyuma, jeshi lilisema Jumapili.

Mpiganaji huyo, Anywari Al Iraq, raia wa Uganda, alikamatwa katika misitu ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambako kundi la waasi la Allied Democratic Forces lina makao yake, jeshi la Uganda People's Defense Forces, lilisema katika taarifa yake.

Wakati wa operesheni hiyo, watu tisa wakiwemo watoto pia waliokolewa kutoka eneo la jimbo la Ituri mashariki mwa Kongo, jeshi lilisema."Aina ya vifaa vya kutengenezea vilipuzi vilivyoboreshwa (IED) vilipatikana," ilisema.

Waasi wa ADF walianza uasi nchini Uganda lakini wamejikita nchini Kongo tangu mwishoni mwa miaka ya 1990.

ADF iliahidi utiifu kwa Islamic State katikati ya 2019 na inashutumiwa kuwaua mamia ya wanakijiji katika uvamizi wa mara kwa mara katika miaka ya hivi karibuni.

Chanzo: Bbc