Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jeshi la Uganda lagoma kuondoka Congo, ADF watajwa

Adsfhsdgfg.png Jeshi la Uganda lagoma kuondoka Congo, ADF watajwa

Fri, 3 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Uganda (UDF) linasema halitaondoka Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, hadi pale waasi wa ADF watakaposhindwa.

Siku ya Alhamisi, wakaazi wa Mashariki mwa DRC wanasema walishuhudia wanajeshi wa Uganda na magari yakivuka mpaka wa Mobili kuingia nchini humo.

Katika hatua nyingine, mateka 28 wakiwemo wanawake watano waliokuwa wameshikiliwa na waasi wa ADF wamefanikiwa kutoroka katika eneo la Luna Etat, baada ya mashambulizi ya jeshi la Uganda dhidi ya waasi hao.

Operesheni za pamoja kati ya DRC na majeshi ya Uganda zinaendelea katika eneo la Beni, katika mkoa wa Kivu Kaskazini. Mashambulizi ya anga na hatua za ardhini zinatekelezwa dhidi ya ngome za kundi la ADF, serikali na jeshi la DRC walithibitisha tangu Jumanne.

Kundi la waasi wa ADF linahusishwa katika mauaji na vitendo vya kikatili dhidi raia wa maeneo ya mpaka na Uganda, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, upande wa mashariki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live