Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jeshi la Sudan lawazuilia watoto 'waliolazimishwa' na RSF kupigana

Jeshi La Sudan Lawazuilia Watoto 'waliolazimishwa' Na RSF Kupigana Jeshi la Sudan lawazuilia watoto 'waliolazimishwa' na RSF kupigana

Mon, 30 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Jeshi la Sudan linasema kuwa limewazuilia watoto ambao "walilazimishwa" kupigana pamoja na Kikosi cha Waasi (RSF) katika mzozo unaoendelea.

Televisheni ya Sudan inayomilikiwa na serikali inasema idadi isiyojulikana ya watoto wanashikiliwa Wadi Saidna, kaskazini mwa Khartoum.

Tarehe 15 Septemba, SAF ilikabidhi watoto 30 waliokuwa wameshikiliwa kama wafungwa wa vita kwa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC).

RSF imekuwa ikishutumiwa mara kwa mara kwa kukiuka sheria za kimataifa kwa kuwaajiri watoto wadogo katika mzozo unaoendelea nchini Sudan.

Wakati huo huo, RSF ilisema Jumamosi kwamba wanajeshi 260 wa jeshi la Sudan walijiunga nao mjini Khartoum.

Mapigano yanaendelea kati ya jeshi na RSF katika mikoa ya Khartoum, Darfur na Kordofan huku kukiwa na ripoti kwamba mazungumzo mapya nchini Saudi Arabia yanalenga kufikia usitishaji mapigano na usaidizi wa kibinadamu.

Chanzo: Bbc