Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jeshi la Sudan latoa malalamiko mashambulizi ya 'Radiamali'

Sudan Yaanza Mazungumzo Ya Kuleta Makundi Ya Jeshi Pamoja Jeshi la Sudan latoa malalamiko mashambulizi ya 'Radiamali'

Thu, 13 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Sudan limesema katika taarifa yake iliyotolewa mapema leo Alhamisi kwamba "Vikosi vya Radiamali ya Haraka" vimepeleka majeshi katika mji mkuu na majimbo ya nchi hiyo bila taarifa yoyote ya awali.

Taarifa iliyotolewa na jeshi la Sudan imeongeza kuwa harakati za Vikosi vya Radiamali ya Haraka ndani ya mji mkuu na majimbo inakiuka majukumu na mfumo wa kazi, na kuonya kuwa nchi hiyo inapitia hatua hatari, na kwamba harakati hiyo itasababisha mivutano zaidi inayoteteresha usalama nchini.

Chanzo cha kijeshi kilisema hapo awali kwamba Vikosi vya Radiamali ya Harakaka vimepeleka idadi kubwa ya askari wake katika mji wa "Merowe" kaskazini mwa Sudan bila kutoa taarifa kwa jeshi, na kwamba wanajeshi kutoka mikoa mingine wamehitajika kwa ajili ya kukabiliana na hali hiyo.

Chanzo hicho kimesema kuwa jeshi la Sudan limevitaka Vikosi vya Radiamali ya Haraka kuondoka katika maeneo ya Merowe ndani ya masaa 24, na ikiwa havitafanya hivyo, vitalazimishwa kuondoka.

Baadhi ya mitandao ya kijamii pia iliripoti kuwa Vikosi vya Radiamali ya Haraka vimechukua hatua za kivita katika uwanja wa ndege wa Merowe.

Raia wa Sudan waliandamana mbele ya ngome ya jeshi la Sudan katika wilaya ya Merowe Jumatano jioni wakionyesha mshikamano wao na jeshi la Sudan.

Ni vyema kutambua kwamba Vikosi vya Radiamali ya Haraka vinafanya kazi chini ya uongozi wa Mohamed Hamdan Dagalo, Makamu wa Rais wa Baraza Kuu la kijeshi linalotawala Sudan, Abdel Fattah Al-Burhan, na vilianzishwa kwa ajili ya kupambana na wanamgambo wa Darfur (magharibi).

Pande mbili zinazozozana nchini Sudan zimechelewesha kutia saini makubaliano ya mwisho ya kisiasa ili kutoa nafasi kwa wanajeshi kufanya mazungumzo zaidi ya kumaliza mgawanyiko unaoshuhudiwa. Kumeripotiwa hitilafu juu ya jinsi ya kujumuishwa vikosi vyote vya jeshi katika jeshi moja la taifa huku wanajeshi waliofanya mapinduzi wakiendelea kung'ang'ania madaraka ya nchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live