Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jeshi la Sudan latangaza kupiga hatua kubwa katika vita na RSF

Sudan RSF Jeshi la Sudan latangaza kupiga hatua kubwa katika vita na RSF

Wed, 21 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Sudan (SAF) limetangaza kupiga hatua kubwa ya kwanza katika miezi 10 ya vita na vikosi hasimu vya Msaada wa Haraka (RSF), na hivyo kuweza kudhibiti tena sehemu ya mji muhimu wa Omdurman.

Hatahivyo vikosi vya RSF, vimepinga tamko hilo na kusema "Jeshi limegeukia propaganda kwani linaelekea kushindwa."

Kundi la RSF limekuwa likipigana na jeshi kwa ajili ya udhibiti wa nchi hiyo ya Kaskazini mwa Afrika tangu mwezi Aprili katika vita vilivyosababisha vifo vya maelfu ya watu na wengine milioni nane kulazimika kuyahama makazi yao huku kukiwa na onyo la njaa.

RSF ilichukua udhibiti wa sehemu kubwa ya mji mkuu Khartoum pamoja na pia miji muhimu ya Omdurman na Bahri. Wakaazi wa miji hiyo wanasema kundi hilo limewafukuza kutoka kwa nyumba zao, kuwapora mali na mali zao, na kuwabaka wanawake.

Kikosi hicho kinashutumiwa kwa uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya ubinadamu, na mauaji ya kikabila katika jimbo la Darfur Magharibi.

Tangu kuanza kwa mwaka huu, jeshi limepata mafanikio baada ya kufanya kampeni pana ya mashambulizi ya anga.

Jeshi lilikuwa limepata vikwazo vingi kutoka kwa Vikosi vya Msaada wa Haraka, huku baadhi wakihusisha maendeleo yaliyofanywa na RSF na " usimamizi wao wa vifaa katika, uungaji mkono makamanda wa wa kieneo, na msaada wa Umoja wa Falme za Kiarabu kupitia nchi Jirani ya Chad.”

Sudan inatawaliwa na Abdel Fattah al-Burhan, ambaye aliingia madarakani kama mkuu wa Baraza la Utawala la Mpito, linaloundwa na wawakilishi wa kijeshi na raia, baada ya kuondolewa kwa mtawala wa muda mrefu Omar al-Bashir 2019.

Kiongozi huyo wa kijeshi alichukua mamlaka kamili katika mapinduzi ya Oktoba 2021, na hivyo kusitisha mchakato wa kukabidhi raia utawlaa kwa mujibu wa mapatano ya baada ya mapinduzi ya 2019.

Mnamo Januari, Burhan alikataa juhudi za upatanisho na RSF, na kuahidi kuendeleza vita vya miezi mingi na kundi hilo hadi ushindi upatikane.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live